Taari yao kwa vyombo vya habari hii leo Yanga imesema kuwa walizuiwa kutumia jezi hizo zenye nembo ya SportPesa kwasababu ni kukosekana kwa maelekezo ya matumizi ya wadhamini hapo awali na hivyo kulazimika kuzibwa kwa sehemu hiyo.
Yanga akiwa ugenini nchini Algeria ilikubali kipigo cha mabao 4 – 0 kutoka kwa wenyeji wao timu ya USM Alger mabao yakifungwa na Darfalou dakika ya nne, Chafai akifunga dakika ya 32, Meziane akitupia dakika ya 54 na lamwisho likiwekwa kimyani na Zemmamouche dakika ya 93.
0 Comments