Bocco
jana alifunga mabao mawili wakati timu yake ikilipa kisasi cha kufungwa
na Mbao bao 1-0 mchezo wa awali uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba huku
wao wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0 uwanja wa Jamhuri.
"Ni
ngumu kupata matokeo kutokana na ushindani uliopo ila kikubwa
kinachotubeba ni ushirikiano uliopo yetu wachezaji pamoja na uongozi
bila kusahau nguvu ya mashabiki tunawaomba waendelee kutupa sapoti
tutaendelea kupambana," amesema Bocco.
Kwenye
vinara wa kutupia TPL, Bocco anashika nafasi ya tatu baada ya kufikisha
jumla ya mabao 11 huku kinara akiwa ni Salum Aiyee wa Mwadui ambaye
ametupia mabao 16.
0 Comments