Mkuu
wa Habari na Mawasiliano wa Mabingwa wa Ligi Kuu (VPL) Simba SC, Haji
Manara amefunguka na kumwagia sifa nyota wa timu ya Taifa ya Ureno,
Cristiano Ronaldo huku akidai mchezaji huyo ndio mtu maarufu ulimwenguni
kote na mtu pekee aliyepigwa picha nyingi tokea alipoumbwa Adam na
Hawa.
Manara ametoa kauli hiyo asubuhi ya leo Juni 16, 2018 baada ya Ronaldo kuingia kwenye 'record' ya kuwa mfungaji wa kwanza kufunga Hat- Trick ya kwanza katika fainali za Kombe la Dunia 2018 kwenye mechi ya Kundi B iliyowakutanisha Ureno dhidi ya Hispania.
"Kuna
mamilioni ya watu wanaocheza soka kote duniani lakini mchezaji bora ni
mmoja tu, Cristiano Ronaldo ndio mwanadamu maarufu kupita wote
ulimwenguni na ndio mtu aliopigwa picha nyingi kupita wote toka
alipoumbwa Adam na Hawa", amesema Manara.
Pamoja
na hayo, Manara ameendelea kwa kusema "hata mitandaoni yeye ndio
anaongoza kwa 'followers' kuliko kiumbe chochote kilicho hai chini ya
jua, mchukie utakavyo ila huyo ndio Cristiano Ronaldo ama 'De le boss wa
Portugal".
Cristiano
Ronaldo ni mchezaji wa tatu wa Ureno kufunga Hat -Trick katika michuano
ya Kombe la Dunia nyuma ya Eusebio na Pauleta ambapo pia Hat -Trick
hiyo ni ya sita kwa timu ya Taifa ya Ureno

0 Comments