Golikipa
wa timu ya taifa ya Iceland, Hannes Þór Halldórsson, amechaguliwa kuwa
mchezaji bora wa mechi katika mchezo wa leo dhidi ya Argentina kwenye
michuano ya Kombe la Dunia.
Halldorsson
amepata tuzo hiyo baada ya kuokoa mipira mingi ya wachezaji wa
Argentina ikiwemo penati ya Lionel Messi, ambayo ilionekana kumaliza
furaha ya mchezaji huyo uwanjani.
Katika mchezo huo, mechi hiyo imeweza kumalizika kwa matokeo ya 1-1 na timu zote kuweza kuambulia alama moja.
Kipa
huyo amemzuia Messi kujibu mapigo ya Hat-Trick aliyoyafanya Ronaldo
jana dhidi ya Spain, Iceland imekuwa taifa dogo zaidi kushiriki kwenye
michuano ya Kombe la dunia.

0 Comments