Kocha
ya kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria, Gernot Rohr amesema kuwa makosa
mengi waliyoyafanya katika mechi dhidi ya Croatia ni chanzo kikuu cha
kipigo cha 2- 0 walichopokea.
Kikosi
hicho maarufu kama ‘Super Eagles’ kilipokea kipigo hicho jana katika
uwanja wa Kaliningrad nchini Urusi ambapo mchezaji wake Oghenekaro Etebo
alijifunga na pia kupokea kipigo cha mkwaju wa penati uliopachikwa na
Luka Modric.
“Tunafahamu
kuwa tulifanya makosa mengi sana ambayo yalikuwa muhimu; na iko wazi
kuwa tunatakiwa kuhakikisha tunayafanyia kazi ili twende mbele,” alisema
kocha huyo.
Aliongeza
kuwa kipigo hicho kimewavunja moyo wachezaji na kwamba wanapaswa
kufanya kazi kiuweledi zaidi watakapokutana na vigogo wengine Argentina
na Iceland.
“Tulijipanga
vizuri na iko wazi kuwa mbinu zetu hazikuwa mbaya. Lakini tunatakiwa
kuhakikisha tunazingatia weledi zaidi kabla ya michezo inayofuata,”
aliongeza.
Aidha,
kocha huyo ambaye amekiri kuwa kupoteza mchezo huo wa jana kunafanya
kazi waliyoianza kuwa ngumu zaidi, alisema kuwa kiwango cha soka
kilichooneshwa na nahodha wa timu hiyo Mikel Obi kilikuwa cha kuridhisha
sawa na kiwango kilichooneshwa na safu ya ulinzi.


0 Comments