Ukiachana na ukongwe wote na heshima aliyoweka Kaseja ndani na nje ya soka la Tanzania, alikuwa hajawahi kucheza mechi za Sports Xtra Ndondo Cup lakini kwa mara ya kwanza alikaa kwenye milingoti ya magoli ya Ndondo Cup kuidakia UV TMK ilipocheza dhidi ya Stim Tosha ‘Stamala’.
“Nilikuwa sijawahi kucheza mashindano ya Ndondo, hii ni mara yangu ya kwanza nacheza. Mashindano hako poa na yanasaidia vijana kuonekana na kuwajengea uzoefu kwa sababu huku wanakutana na wachezaji wengi wenye uzoefu na mbinu nyingi”-Juma Kaseja.
Kaseja aliiongoza UV TMK kushinda 3-0 dhidi ya Stim Tosha katika mchezo wake wa kwanza Ndondo Cup.

0 Comments