Na Magdalena Kashindye
Mashindano ya vijana wa timu za ligi kuu Tanzania bara walio chini ya umri wa miaka 20 kuendelea leo jijini Dodoma.
Michezo
miwili itapingwa katika viwanja vya chuo kikuu cha Dodoma na mchezo wa
kwanza utazikutanisha timu za Mbao FC ya jijini mwanza na Azam FC ya
jijini Dar es Salam majira ya saa 8:00 mchana.
Mbao
ilitinga hatua ya robo fainali kwa kumaliza kinara wa kundi A kwa I
pointi 5 na Azam alimaliza wa katika nafasi ya pili kutoka kundi C kwa
pointi 5.
Mchezo
wa pili utapingwa saa 10:15 Kati ya mtibwa sugar ya morogoro na Ruvu
shooting ya pwani. Mtibwa aliingia hatua ya robo fainali kwa kumaliza
kinara wa kundi C kwa pointi 5 huku Ruvu shooting alimaliza kwa kushika
nafasi ya pili kutoka kundi A.
Washindi wa leo wataingia hatua ya nusu fainal.

0 Comments