Ufaransa
imefanikiwa kuibuka na ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Kombe
la Dunia mwaka huu nchini Urusi wa mabao 2-1 dhidi ya Australia.
Mabao
ya mchezo huo yametiwa kimiani na Antoine Griezmann katika dakika ya 58
kwa njia ya mkwaju wa penati na la pili likitiwa kimiani na Paul Pogba .
Bao pekee la Australia liliwekwa wavuni na Mile Jedinak mnamo dakika ya 62 kwa mkwaju wa penati.
Mechi hii imekuwa ya kwanza kushuhudiwa penati mbili ndani ya dakika 90 zikipigwa kwa pande zote.
Ushindi
huu wa Ufaransa unawapa alama tatu muhimu kwenye kundi C ambapo baadaye
Peru na Denmark watakuwa wanacheza pia kutoka kundi hilo.



0 Comments