Kindoki
aliokoa penalti mbili kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Alliance
FC uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba hali iliyofanya Yanga kutinga hatua
ya nusu fainali kwa ushindi wa penalti 4-3 ambapo itakutana na Lipuli ya
Iringa Uwanja wa Samora mwezi huu.
"Hatua
nzuri ambayo nimefikia kwa sasa, ninamshukuru Mungu kwa kunipa nguvu na
uvumilivu hasa katika kipindi kigumu ambacho nimepitia ila yote ni
kheri kwangu kwani ni furaha kubwa sana hapa Yanga.
"Mashabiki
ni watu muhimu kwangu nawashukuru kwa sapoti yao na kunipa muda wa
kufanya mengi zaidi, ninawaahidi kufanya mengi makubwa wazidi kunipa
sapoti," amesema Kindoki.
Kindoki
alianza kwa kuruhusu 'hat-trick' mchezo wake wa kwanza dhidi ya Stand
United uliochezwa Uwanja wa Taifa licha ya Yanga kushinda kwa mabao 4-3.

0 Comments